Hii ni makala ya kwanza katika mfululizo wa mafunzo ya Jinsi ya Kutengeneza Website. Karibu ujifunze! Website ni nini? Kwa Kiswahili tunaita tovuti au wavuti ingawa katika mafunzo haya tumetumia neno website kwani ndio linalofahamika na wengi na hivyo itakuwa rahisi kwa watu kufahamu nini tunakizungumzia. Website ni mtandao ambao unatengenezwa kwa lengo la kuweka data au taarifa za aina mbalimbali (Usichanganye na Blog ambayo taarifa huwekwa kwa njia ya makala). Mtu anaweza kutengeneza Website kwa ajili ya kuweka taarifa za biashara yake katika mfumo wa kurasa , au kutoa elimu au kufundishia. Website inakuwa na Kurasa ya nyumbani (Homepage) ambayo baada ya mtu kuingiza anuani tu anafikia. Katika ukurasa wa nyumbani kunawekwa taarifa za msingi kuhusu website na taarifa nyingine huwekwa katika kurasa nyingine ambazo zinaweza kufikika kiurahisi kupitia links zilizowekwa au katika MENU. Mifano ya Website ni kama https://necta.go.tz n.k. Katika sehemu hi...