Hii ni makala ya kwanza katika mfululizo wa mafunzo ya Jinsi ya Kutengeneza Website. Karibu ujifunze!
Website ni nini?
Kwa Kiswahili tunaita tovuti au
wavuti ingawa katika mafunzo haya tumetumia neno website kwani ndio
linalofahamika na wengi na hivyo itakuwa rahisi kwa watu kufahamu nini
tunakizungumzia.
Website ni mtandao ambao
unatengenezwa kwa lengo la kuweka data au taarifa za aina mbalimbali
(Usichanganye na Blog ambayo taarifa huwekwa kwa njia ya makala).
Mtu anaweza kutengeneza Website kwa ajili ya
kuweka taarifa za biashara yake katika
mfumo wa kurasa, au kutoa elimu au kufundishia.
Website inakuwa na Kurasa ya
nyumbani (Homepage) ambayo baada ya mtu kuingiza anuani tu anafikia.
Katika ukurasa wa nyumbani
kunawekwa taarifa za msingi kuhusu website na taarifa nyingine huwekwa katika
kurasa nyingine ambazo zinaweza kufikika kiurahisi kupitia links zilizowekwa au
katika MENU.
Mifano ya Website ni kama https://necta.go.tz n.k.
Katika sehemu hii ya kwanza utajifunza
mambo ya muhimu unayotakiwa kufahamu kabla hujaanza kutengeneza Website.
Usihofu hakuna ugumu wowote!
Mambo ya Muhimu Unayotakiwa
Kufahamu Kabla Hujaanza Kutengeneza Website.
1.Domain na usajili wake: Domain ni jina au anuani ya website yako
ambayo watu wataandika watakapotaka kutembelea katika website yako, mfano www.jina.co.tz
Kuna domain za aina mbalimbali kama .com, .org, .online, .net, .co.tz,
.go.tz, na kadhalika. Domain zinasajiliwa katika kampuni mbalimbali zilizopo
nchini au hata nje ya nchi. Mfano wa Kampuni zinazotoa huduma hizo kwa Tanzania
ni Yatosha, Duhosting, Extreme Web na nyenginezo. Kampuni maarufu ya nje
unayoweza kusajili domain ni Godaddy (zipo nyingine pia).
2. Hosting: Hii ni huduma ya kurusha website yako hewani, yaani ili
website yako iwe mtandaoni na watu waweze kuifikia ni lazima ifanyiwe hosting
ambayo inakupatia nafasi ya kuhifadhi taarifa za website yako. Pia huduma ya
hosting inakupatia CPANEL(Control Panel)
ambayo utaitumia kucontrol website na mafaili yako.
3. Ufahamu wa Lugha za kimtandao (codes) angalau HTML na CSS itakuwa
vizuri zaidi ukifahamu na Javascript na PHP. Usijali, hii namba tatu sio lazima
hata kama haujui chochote kati ya vitu hivyo nilivyovitaja bado unaweza
kutengeneza Website Bila Tatizo lolote.
Ni muhimu kujua codes (HTML na
CSS) kama unataka kuwa mtaalamu zaidi katika Website Design.
Unaweza kujifunza HTML na CSS kwa
urahisi zaidi kupitia Viungo vilivyopo hapa chini
HTML
https://www.w3schools.com/html/
https://www.tutorialspoint.com/html/index.htm
CSS
https://www.w3schools.com/css/default.asp
https://www.tutorialspoint.com/css/index.htm
Kama una swali lolote unaweza
kuuliza hapo chini.
Comments
Post a Comment